Date: 
14-02-2023
Reading: 
Mwanzo 49:8-10

Jumanne asubuhi tarehe 14.02.2023

Mwanzo 49:8-10

8 Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.

9 Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?

10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.

Neno la Mungu lina nguvu;

Yusufu alikuwa akiishi na kutawala Misri akiwa na ndugu zake. Yakobo baba yao alipokuwa mzee aliwabariki na kuwapa usia watoto wake. Somo tulilosoma ni sehemu ya baraka ya Yakobo kwa watoto wake. Anambariki Yuda akifananisha kama simba, mnyama jasiri. Anamtamkia Yuda ukuu katikati ya Taifa la Mungu. Na baadaye Yuda lilikuja kuwa kabila kubwa katika Israeli.

Wakati wa Agano la kale wazazi waliwabariki watoto wao, na baraka yao ilikuwa kweli baadaye katika Bwana. Kwa zama hizi za Agano jipya, Yesu Kristo hutubariki pale tunapomwamini kwa njia ya neno lake, ambalo ndiyo hutupa dira ya kuishi maisha ya kumpendeza yeye. Lishike neno la Mungu ili upate baraka zake. Siku njema.

Heri Buberwa