Date: 
13-05-2022
Reading: 
Neno la Mungu Leo Hii

Isaya 25:6-8

----------------------------------------

6 Na katika mlima huu Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.
7 Naye katika mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote.
8 Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo.

Maisha mapya ndani ya Yesu;

Israeli walikuwa Yerusalemu  wakipewa maelekezo na Bwana ili wasije kwenda utumwani. Somo la asubuhi hii ni sehemu ya maelekezo waliyopewa, akiahidi kuwapa karamu ya vinono. Kwa tafsiri pana, alikuwa akiwaahidi mema, iwapo wangemtii na kumcha yeye.

Siku zote Mungu anatuita kumtii na kumsikia ili atupe mema ya nchi. Ni kwa kumsikia anaponena nasi kupitia neno lake, na kuishi tukitenda  mema, ndipo tunakuwa na maisha mapya katika Yesu Kristo.