Date: 
13-07-2023
Reading: 
Marko 2:13-17

Alhamisi asubuhi tarehe 13.07.2023

Marko 2:13-17

13 Akatoka tena, akaenda kando ya bahari, mkutano wote ukamwendea, akawafundisha.

14 Hata alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.

15 Hata alipokuwa ameketi chakulani nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwa maana walikuwa wengi wakimfuata.

16 Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

17 Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Mtu akinitumikia na anifuate;

Yesu aliingia Kapernaumu akaingia kwenye nyumba. Watu walijaa pasiwe na nafasi hata kidogo. Mara akaletwa mgonjwa kwenye kitanda, waliombeba walitoboa dari ili kumfikia Yesu. Yesu alipoona imani ya waliombeba mgonjwa, akamponya yule mgonjwa wao.

Baada ya pale ndipo Yesu akamwita Lawi aliyekuwa ameketi forodhani amfuate. Akaingia nyumbani mwake kula chakula na wote waliokuwepo, miongoni mwao watozaushuru na wenye dhambi. Waandishi na Mafarisayo walipata shida kwa Yesu kula meza moja na watoza ushuru na wenye dhambi! Ukizingatia walikuwa bado wanakumbuka alivyomwambia mgonjwa tuliyemuona hapo juu kwamba "umesamehewa dhambi zako". Walishangaa kuhusu mamlaka ya Yesu!

Kumbe Yesu yeye alikuja kwa ajili ya watu wote kama tulivyosoma mstari wa 17, ndiyo maana hakuchagua watu wa kula nao chakula wala kuponya. 

Hata sasa Yesu hachagui, anatuita sote tumtumikie na kumfuata. Tudumu katika imani yetu tukimtumikia na kumfuata siku zote za maisha yetu. Amina.

Alhamisi njema.

Heri Buberwa