Date: 
16-09-2023
Reading: 
Mathayo 17:24-27

Jumamosi asubuhi tarehe 16.06.2023

Mathayo 17:24-27

24 Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa.

25 Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni?

26 Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru.

27 Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.

Uwakili wetu kwa Bwana;

Yesu aliingia Kapernaumu, watozao shekeli wakaogopa kumwendea moja kwa moja wakamtumia Petro kuuliza kama Yesu hutoa nusu shekeli. Yesu alimuuliza Simoni kama alitakiwa kulipa shekeli (kodi) akamwelekeza kuvua samaki ili akalipe kodi husika.

Yesu aliwajibika kulipa shekeli katika jamii ile.

Alitimiza wajibu 

Nasi tunaalikwa kutimiza wajibu wetu katika maisha yetu tukitenda yatupasayo. Tutimize wajibu wetu kwa Bwana kama mawakili wema. Amina.

Uwe na Jumamosi njema.

Heri Buberwa