Date: 
16-10-2023
Reading: 
Matendo 5:12-16

Jumatatu asubuhi tarehe 16.10.2023

Matendo ya Mitume 5:12-16

12 Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;

13 na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha;

14 walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake;

15 hata ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao.

16 Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.

Imani isiyo na mashaka;

Sura ya 5 ya Matendo ya Mitume inaanza kwa kusimulia kisa na Anania na Safira, waliouza kiwanja chao wakapeleka fedha ya kiwanja pungufu hekaluni. Walidhani wamewadanganya mitume, kumbe walikuwa wanamdanganya Mungu. Walikufa pale pale mbele ya Mitume.

Baada ya hapo, ndipo somo la asubuhi ya leo linaonesha watu wakiamini Injili iliyohubiriwa na Mitume. Mstari wa 14 unaonesha kwamba waamini waliongezeka kwa Bwana. Kumbe Injili tunayohubiriwa ndiyo neno la Mungu, linalotoka kwa Mungu mwenyewe. Tukiliamini tunakuwa na Imani isiyo na mashaka. Amina.

Tunakutakia wiki njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri