Date: 
27-10-2023
Reading: 
Mithali 16:1-3

Ijumaa asubuhi tarehe 27.10.2023

Mithali 16:1-3

1 Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.

2 Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huzipima roho za watu.

3 Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.

Suleimani anaonesha rehema ya Mungu kwa mwanadamu wakati wote, kama Baba na muumbaji. Suleimani anaandika kwamba moyo waweza kutamani na kupanga mambo mengi, lakini awezaye kujibu kwa kweli ni Mungu tu. Ndiyo maana Suleimani anasema njia za mtu zinaweza kumpendeza mtu mwenyewe, lakini Bwana huzipima roho zao. 

Katika yote hayo mkazo ni kumkabidhi Bwana kazi zetu,na mawazo yetu yatathibitika. Ni kwa sababu mawazo yetu ndiyo hutuelekeza tufanye nini ili kupata matokeo. Tukimkabidhi Bwana kazi zetu tutakuwa na matokeo mazuri. Kumbe wito kwetu hapa ni kumkabidhi Bwana maisha yetu siku zote, ili tuwe na mwisho mwema. Tuheshimu wito huu. Amina.

Ijumaa njema.

Heri Buberwa