Date: 
04-01-2024
Reading: 
Yohana 14:13-14

Alamisi asubuhi tarehe 4/01/2024

Yohana 14:13-14

13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.

14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya

Tuanze yote katika jina la Yesu Kristo.

Yohana ameandika maneno Yesu aliyoyasema kwa wafuasi wake. Nasi kama wafuasi wa Yesu wa wakati huu, maneno hayo yanatuhusu. Neno linatuhimiza kuwa na imani isiyo na shaka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Pia tunapewa matumaini kuwa tunaye wa kutusaidia wakati wote tukimwiita kwa imani. 

Siku njema.

Mzee C. Swai

.