Date: 
29-01-2024
Reading: 
Mwanzo 41:37-40

Jumatatu tarehe 29/01/2024 asubuhi

Mwanzo 41:37-40

37 Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote.

38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?

39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.

40 Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.

Wokovu wetu ni kwa neema.

Ukisoma mistari iliyotangulia somo la leo, utaona Yusufu alikuwa amefungwa gerezani kwa mashtaka ya uongo. Baadae akatafsiri ndoto ya  mfalme iliyowashinda wote. Ndipo katika somo la leo tunaona akitunikiwa cheo cha juu katika utawala wa mfalme Farao.

Yusufu alipokuwa amefungwa aliendelea kumtumaini Mungu wake, hadi Pharao akapata habari za imani yake. Mungu alimwokoa Yusufu kutoka gerezani na kumweka mahali pa juu kwa imani.

Nasi tuelewe kuwa tunaokolewa kwa imani na si kwa matendo yetu. Tuendelee kuweka tumaini letu kwa Bwana.

Siku njema.