Date: 
06-03-2024
Reading: 
Isaya 55:6-7

Hii ni Kwaresma 

Jumatano asubuhi 06.03.2024

Isaya 55:6-7

6 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;

7 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.

Tumtazame Bwana aliye tumaini letu;

Asubuhi ya leo tunasoma juu ya faraja ya Mungu kwa Israeli walipokuwa utumwani. Tunasoma ahadi ya Mungu juu ya kuwa kwao, akiwaambia kumtafuta yeye wakati wote. Tunasoma pia juu ya ahadi yake ya kuwasamehe dhambi zao mara watubupo dhambi zao. Kwa kifupi anawaalika kutubu dhambi akiahidi kuwasamehe.

Ahadi ya kusamehewa dhambi hudumu hata sasa kwa njia ya Yesu Kristo. Yesu Kristo ndiye hutusamehe dhambi pale tunapotubu.

Hivyo tunaalikwa kumtazama Bwana aliye tumaini letu kwa msamaha wa dhambi ili tuwe na mwisho mwema katika yeye. Amina

Jumatano njema 

 

Heri Buberwa