Date: 
14-03-2024
Reading: 
Isaya 51:9-11

Hii ni Kwaresma 

Alhamisi asubuhi tarehe 14.03.2024

Isaya 51:9-11

9 Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.

10 Si wewe uliyemkata-kata Rahabu? Uliyemchoma yule joka? Si wewe uliyeikausha bahari, Na maji ya vilindi vikuu; Uliyevifanya vilindi kuwa njia, Ili wapite watu waliokombolewa?

11 Nao waliokombolewa na Bwana watarejea, Watafika Sayuni, wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; Watapata shangwe na furaha; Huzuni na kuugua zitakimbia.

Furahini katika Bwana siku zote;

Taifa la Mungu wanapewa ujumbe wa kuwa na nguvu katika Bwana, maana ukombozi upo kwa ajili yao. Mstari wa 11 ni ahadi ya ukombozi kwa Israeli kurejea katika nchi yao (kumbuka hapa walikuwa utumwani). Wanaahidiwa shangwe na furaha ya milele pasipo na huzuni.

Sisi tunayo furaha ya milele, kwa sababu Yesu aliteswa na kufa kwa ajili yetu. Yaani tunayo hakika ya kuurithi uzima wa milele, tukidumu katika yeye na kutenda yatupasayo. Kristo ndiye mwenye hatma yetu, hivyo tumwamini, tumsikie na kumcha ili furaha yake idumu ndani yetu kuelekea uzima wa milele. Amina.

Alhamisi njema 

Heri Buberwa