Date: 
04-05-2024
Reading: 
Yeremia 20:13

Jumamosi asubuhi tarehe 04.05.2024

Yeremia 20:13

Mwimbieni Bwana; msifuni Bwana; Kwa maana ameiponya roho ya mhitaji Katika mikono ya watu watendao maovu.

Njooni tumwimbie Bwana;

Yeremia alipitia wakati mgumu katika safari ya imani. Ilihusisha kupoteza mali yote na familia. Lakini katika yote hakuwahi kumkosea Mungu. Alizidi kuimarika katika imani hata pale aliposhawishiwa na mke wake kumkufuru Mungu. Mstari wa somo ni sifa kwa Mungu, Yeremia akiimba wimbo wa sifa kwa Mungu aponyaye.

Safari ya imani huwa siyo nyepesi maana siyo ya mteremko tu. Imejaa furaha, lakini pia zipo nyakati za shida. Nyakati zote tunazopitia zisituondoe katika njia ya imani, maana Kristo tumuaminiye ndiye tegemeo na kiongozi wetu. Tumsifu Bwana atuwezeshaye katika yote kwa kutenda yatupasayo. Amina.

Jumamosi njema 

 

Heri Buberwa