Date:
15-05-2025
Reading:
Mathayo 9:32-34
Hii ni Pasaka
Alhamisi asubuhi tarehe 15.05.2025
Mathayo 9:32-34
32 Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo.
33 Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena, makutano wakastajabu, wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.
34 Lakini Mafarisayo wakasema, Kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa pepo.
Ndani ya Yesu kuna maisha mapya;
Asubuhi ya leo tunasoma Yesu akimponya mtu bubu, mwenye pepo pia. Hadi analetwa kwa Yesu bila shaka alikuwa ameteswa na pepo muda mrefu bila msaada, akiwa bubu. Lakini Yesu kwa huruma na upendo wake alimponya, akaweza kunena baada ya pepo kumtoka. Makutano walibaki kushangaa yaliyotokea, huku Mafarisayo wakisema kuwa Yesu alitoa pepo kwa nguvu za mkuu wa pepo!
Tunaona mtu aliyeponywa na Yesu akiweza kunena baada ya kutokwa na pepo. Kwa tafakari ya wiki hii, naweza kusema kuwa yule ndugu aliyeponywa maisha yake yalikuwa mapya baada ya kutolewa pepo, akanena. Jambo la muhimu ni kuwa aliponywa na Yesu Kristo, yaani maisha yake yalikuwa mapya kwa njia ya Yesu Kristo. Nasi tukikaa ndani ya Yesu maisha yetu yanakuwa mapya daima. Amina
Alhamisi njema
Heri Buberwa