Date: 
21-12-2021
Reading: 
Sefania 3:14-17

Hii ni Advent 

Jumanne asubuhi tarehe 21.12.2021

Sefania 3:14-17

14 Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli; Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti Yerusalemu.
 
15 Bwana ameziondoa hukumu zako, Amemtupa nje adui yako; Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana, yu katikati yako; Hutaogopa uovu tena.
 
16 Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa, Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee.
 
17 Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.

Bwana yu Karibu;

Asubuhi hii tunasoma unabii wa kale unaoonesha Yesu kuingia Yerusalemu kwa ajili ya kuokoa watu wake. Alitabiriwa kuja katikati ya watu wake, akiwa shujaa wao na kuwaokoa.

Yesu huyu aliyetabiriwa alikuja kama mwanadamu kukaa kwetu, na atarudi tena kwa utukufu kulichukua Kanisa. Tusiogope. Uzima wa milele umeandaliwa kwa ajili yetu. Tujiandae kumpokea Bwana, maana yu karibu.

Siku njema.