Date: 
23-11-2021
Reading: 
Waebrania 11:13-16

Jumanne asubuhi 23.11.2021

Waebrania 11:13-16

[13]Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.

[14]Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe.

[15]Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.

[16]Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.

Uzima wa Ulimwengu ujao;

Somo la leo asubuhi ni sehemu ya pili ya imani katika waraka kwa Waebrania, inayoangazia imani ya Ibrahimu na Sarah. Hawa wazee waliishi kwa imani hadi kufa kwao wakaipokea ahadi ya Bwana.

Ni wito wangu kwako kuishi katika imani kama ulivyompokea Yesu pale ulipomkiri kwa njia ya sakramenti ya ubatizo, ili uwe na mwisho mwema ukiipokea ahadi ya Bwana, yaani uzima wa milele.

Siku njema.