Date: 
28-03-2023
Reading: 
Waebrania 9:23-28

Jumanne asubuhi tarehe 28.03.2023

Waebrania 9:23-28

23 Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.

24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;

25 wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake;

26 kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.

27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;

28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.

Yesu ni Mpatanishi;

Zamani za Agano la kale makuhani waliingia hekaluni kila mwaka kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi za watu. Yesu hakufa mara nyingi ili kutupatanisha na Baba, alikufa mara moja tu msalabani na upatanisho ukapatikana. 

Yesu alitolewa sadaka mara moja ili azichukue dhambi za ulimwengu. Anatualika kumwamini na kumfuata maana yeye ndiye mpatanishi wetu na Mungu. Kwake uko uzima. Tuendelee kumtazamia Bwana aliye wokovu wetu kuelekea uzima wa milele.

Siku njema.

Heri Buberwa