Date: 
09-02-2023
Reading: 
Warumi 9:12-24

Alhamisi asubuhi tarehe 09.02.2023

Warumi 9:19-24

19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake?

20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?

21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?

22 Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;

23 tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu;

24 ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia?

Tunaokolewa kwa neema;

Mtume Paulo anaongelea neema na ghadhabu ya Mungu, kwamba Mungu huwajalia neema yake watu wote. Paulo anaonesha kwamba hakuna asiye na mamlaka juu ya kitu chake. Kwa Mungu kutuumba na kutuwezesha kila siku, hiyo tayari ni neema. Lakini ni muhimu kujitazama mwenendo wetu ili ghadabu ya Mungu isiwe juu yetu maana yeye anayo mamlaka kwetu.

Paulo anatuita kutambua kuwa sisi ni mali ya Mungu, naye anayo mamlaka juu yetu. Mungu ametupa wokovu kwa neema, lakini hiyo haiondoi sisi kutimiza wajibu wetu yaani kumcha. Tukimcha Bwana neema yake inakaa juu yetu, yaani tunadumu katika wokovu. Lakini tukimuasi Bwana ghadhabu yake inakuwa juu yetu. Neema yake inatukumbusha kudumu katika yeye aishiye na kutawala, sasa na hata milele. Amina.

Uwe na Alhamisi njema.

 

Heri Buberwa