Date: 
25-05-2022
Reading: 
Yakobo 5:16-18

Jumatano asubuhi tarehe 25.05.2022

Yakobo 5:16-18

16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.

18 Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.

Ombeni katika jina la Yesu Kristo nanyi mtapewa;

Sehemu ya waraka tuliyosoma inatukumbusha kwenda mbele za Mungu kuomba kwa toba. Kwamba maisha yetu yawe ya toba, ndipo twende mbele za Mungu kwa haki. Haki hutufanya tujibiwe sala zetu kama ilivyotokea kwa Eliya.

Itukumbushe kutubu dhambi zetu kwa Mungu wetu, ili tumwendee kwa haki pale tunapompelekea haja zetu. Kumbe maisha ya toba ni muhimu katika maisha yetu, tukiwasamehe wenzetu ili nasi Mungu atusikie.

Siku njema.