Event Date: 
07-04-2021

Akitoa neno la siku Baba Askofu, Dkt. Alex Malasusa alisema kuwa ufufuo wa Yesu Kristo ni ishara tosha juu ya uweza mkuu wa Mungu, na kwamba uweza wake huo hauwezi kuzuiwa na jambo lolote. “Kama Yesu asingefufuka basi imani yetu ingekuwa bure. Inawezekana mpaka leo kuna watu hawaelewi maana ya ufufuo japokuwa wanasherehekea Pasaka na kujazana makanisani. Ufufuo wa Yesu Kristo sio tu suala la kihistoria bali ni suala ambalo ni endelevu katika maisha yetu ya kila siku,” alisema Baba Askofu Malasusa.

Angalia Picha nyingine hapa https://drive.google.com/drive/folders/16BPLz8tolVT39tm4tnXbq8217jnwtTSM...