Date: 
21-03-2023
Reading: 
Yeremia 15:15-16

Hii ni Kwaresma 

Jumanne asubuhi tarehe 21.03.2023

Yeremia 15:15-16

15 Ee Bwana, unajua wewe; unikumbuke, unijilie, ukanilipie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na mashutumu.

16 Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi.

Yesu ni chakula cha uzima;

Nabii Yeremia anamuita Bwana amkumbuke, asimuache. Anamuomba amlipie kisasi kwa wote wanaomuudhi. Yeremia anaomba kudumu katika uvumilivu katika kazi yake ya unabii. Anakiri kuifanya kazi ya Mungu kwa njia ya neno lake, maana aliipokea kwa neno. Yeremia anaandika akionesha uhakika wa Mungu kuwa na yeye katika wito wake.

Ujumbe toka kwa Yeremia ni kumtegemea Bwana katika kazi zetu. Tumeitwa kumwamini na kumtumikia Bwana kwa njia ya neno lake. Tukilishika neno la Mungu, Yesu Kristo anakaa ndani yetu, anatuwezesha kumwamini na kumtumikia kwa utukufu wake.

Mwamini Yesu aliye chakula cha uzima, yaani Mwokozi wa Ulimwengu.

Siku njema.

Heri Buberwa