Date: 
20-11-2021
Reading: 
Yoeli 2:1-2

Jumamosi asubuhi 20.11.2021

Yoeli 2:1-2

[1]Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia;
 
[2]siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.

Hukumu ya mwisho;

Nabii Yoeli alipaza sauti juu ya hukumu ya mwisho, akisema siku ya BWANA inakuja, inakaribia. Kwa maana nyingine Yoeli aliwataka watu kujiandaa na siku ya hukumu.

Ndiyo, ipo siku ya hukumu. Yesu atakuja kuwahukumu walio hai na wafu. Kumbuka kuwa hukumu hii haina upendeleo, bali kila mmoja atahukumiwa kulingana na alivyoishi. Maisha yako ndiyo yatafanya uhukumiwe kulingana na ulivyoishi. Tafakari mwenendo wako kuelekea hukumu ya mwisho, kama utaingia uzimani au la, na uchukue hatua stahiki.

Siku njema.