Date: 
25-11-2021
Reading: 
Yoeli 3:17-21

Alhamisi asubuhi 25.11.2021

Yoeli 3:17-21
[17]Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.
[18]Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya BWANA, na kulinywesha bonde la Shitimu.
[19]Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.
[20]Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi.
[21]Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana BWANA ndiye akaaye Sayuni.

Uzima wa Ulimwengu ujao;

Nabii Yoeli anatabiri juu ya utukufu wa Bwana ujao, kuwa pamoja na yote, Bwana ndiye atamiliki milele. Katika kuwakomboa Israeli, Bwana atabaki mwenye haki, akiwaadhibu wote waliotenda dhambi.

Fanya yote, lakini kumbuka utukufu ni wa Bwana tu, sasa na hata milele. Yeye ndiye atakaa kwenye kiti cha enzi akitawala na kutoa hukumu ya haki. Jiandae kwa ajili ya uzima wa baadae, kwa kutenda mema.
Siku njema