Date: 
22-04-2022
Reading: 
Yona 2:1-10

Hii ni Pasaka;

Ijumaa asubuhi 22.04.2022

Yona 2:1-10

1 Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki,

2 Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu.

3 Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.

4 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.

5 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu;

6 Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu,

7 Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu.

8 Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe;

9 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana.

10 Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.

Tembea na Yesu mfufuka;

Sura ya kwanza ya kitabu cha Yona inasimulia jinsi Yona alivyotumwa Ninawi na Mungu akakataa, akapanda meli kwenda Tarshishi. Meli iliyumba sana, baadaye wasafiri wakamtupa baharini, akamezwa na samaki.

Ndipo somo la leo asubuhi tunamsoma Yona akitubu kwa Bwana kwa kukaidi wito wa kwenda Ninawi. Anajuta akimlikia Mungu, pia anaahidi kumtolea sadaka (9).

Yona alimezwa na samaki kwa sababu hakutii sauti ya Mungu, hadi alipotubu. Ni wazi kuwa bila kutembea na Yesu mfufuka tunakuwa hatarini bila msaada. Usisubiri kumezwa na samaki kama Yona, tembea na Yesu mfufuka.

Siku njema.