Date: 
19-11-2021
Reading: 
Yuda 1:14-16

Ijumaa asubuhi 19.11.2021

Yuda 1:14-16

[14]Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,

[15]ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.

[16]Watu hawa ni wenye kunung’unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.

Hukumu ya mwisho

Jumapili tuliona kuwa Yuda aliandika waraka akionya juu ya uasi uliofanywa na watu, na kuwa chukizo mbele za Mungu. Leo asubuhi tunaona mwendelezo wake, akiandika kuwa Mungu atawaadhibu wote wasiomcha Mungu katika kazi zao, maana ni wenye kiburi, wanung'unikaji, wakitumia vyeo vyao kunyanyasa wengine.

Tunakumbushwa kutumia nafasi zetu kwa utukufu wa Mungu, tukimshuhudia kwa matendo yetu. Watu wapate nafuu ya maisha kupitia kwetu, na siyo maumivu. Tumwakilishe Mungu kwa kutenda haki, ili tusije kuadhibiwa na BWANA siku akirudi.

Siku njema.