Date: 
26-07-2022
Reading: 
Yuda 1:19-25

Jumanne asubuhi tarehe 26.07.2022

Yuda 1:19-25

[19]Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.

[20]Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,

[21]jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.

[22]Wahurumieni wengine walio na shaka,

[23]na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.

[24]Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;

[25]Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina.

Amri mpya nawapa, Mpendane 

Waraka wa Yuda huwaonya walimu wa uongo kwa kuwatangazia hukumu, ukirejea historia ya watu walioangamia kwa kutomcha Bwana. Yuda analisihi Kanisa kujijenga kiimani, na kuomba rehema ya Mungu katika Roho Mtakatifu. Ni wito kwa Kanisa kudumu pendoni, ikingojewa ahadi ya uzima wa milele.

Mafundisho ya uongo yako mengi leo. Ole wake afundishaye uongo! Tuyaepuke mafundisho ya uongo kwa msaada wa Bwana, tukijilinda katika pendo la Mungu hata tupate uzima wa milele.

Siku njema.