Date: 
20-12-2023
Reading: 
1 Wakorintho 9:16-23

Hii ni Advent

Jumatano asubuhi tarehe 20.12.2023

1 Wakorintho 9:16-23

16 Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!

17 Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili.

18 Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.

19 Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.

20 Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria.

21 Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.

22 Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.

23 Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.

Itengenezeni njia ya Bwana;

Mtume Paulo anaandika akisema ole wake asipoihubiri Injili. Anaonesha kwamba kuhubiri injili kwake ni lazima, maana ni kazi aliyotumwa kuifanya ili watu wa Mungu waokoke. Paulo anaenda mbele akisema kuwa alijifananisha na aliowahubiria ili awahubirie waokoke. Maana yake alitumia njia ambazo zingemuwezesha kuhubiri injili ambayo ingemzalia Bwana matunda, yaani watu waokoke.

Ujumbe wa Mtume Paulo hapa kwetu ni uwajibikaji. Paulo anatukumbusha kuitenda kazi ya Mungu kwa bidii, bila kuchoka, kwa matokeo, kwa msaada wa Mungu. Uwajibikaji wetu uende zaidi ya kutenda kazi, kwamba maisha yetu yote yawe ni katika Kristo. Yaani tuitende kazi yake, akiwa ndani yetu, ili tuwe na mwisho mwema. Amina.

Jumatano njema 

 

Heri Buberwa