Date: 
16-06-2022
Reading: 
1 Yohana 5:6-9

Alhamisi asubuhi tarehe 16.06.2022

1 Yohana 5:6-9

6 Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.

7 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.

8 Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja.

9 Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.

Mungu mmoja;

Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Yesu anatambulishwa kama Kristo aliyeshuka toka mbinguni, akiwa Mungu kweli na mwanadamu kweli. Ushuhuda huu ni wazi tangu awali katika imani, maana Kristo hutenda kazi kama Mungu wa Utatu. Mstari wa 10 unatuelekeza kumwamini;

1 Yohana 5:10: Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake.

Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.

Tusipoamini Kristo kama Mungu wa utatu tunakuwa waongo, maana ushuhuda katika hilo unaishi. Endelea kusimama katika Yesu Kristo aliye Mungu kweli katika utatu Mtakatifu.

Siku njema.