Tunaposema kusifu na kuabudu tunamaanisha tunamtukuza mungu kwa njimbo na mapambio, kusifu ni aina fulani ya uimbaji ambayo inasikika au kujulikana kwa jinsi nyimbo zilivyo yaani kuimba kwa unyenyekevu na kwa utulivu.

Mwezi Mei 2014, tumewatembelea vijana ambaao wametoka katika makanisa mbalimbli ya jijini Dar es salaam na kuunda kundi la kusifu na kuabudu linalojulikana kama Morning Glory Team.

Team hii mpaka sasa ina miaka saba katika huduma yake ya kusifu na kuabudu, timu hii ilianza kama mchicha ikiwa na watu wawili nampaka sasa inawatu wasiopungua 15, kati ya hao tisa wanapiga vyombo mbalimbali na kuimba pia.

Timu hii mpaka sasa ina malengo ya kuandaa albamu yao ya kwanza ambayo kwa sasa ipokatika mchakato wa awali.

morning glory1

Albamu hiyo itakuwa na nyimbo 12 ambazo zitatoka katika kibabu cha nyimbo za Tenzi, baadhi ya baadhi ya nyimbo  zitakazokuwa katika albamu hiyo ni Chakutumaini Sina, Bwana usehemu yangu, Twasoma ni njema sana, Ni wako wewe, Yesu kwetu ni rafiki, Njooni kwa mponya njooni leo, Kazi yako ikiisha, Nimesikia Mbiu, Haleluya ame, na nyingine nyingi.

Mmoja kati ya vijana kutoka katika Team Glory ambaye anatambulika kwa jina la Osward Marafyale maarufu kama Jomba, alisema kwamba wanatarajia kufanya kitu ambacho hakijawahi kutokea katika nyimbo za kuabudu na kusifu kwa sababu wamejiandaa vya kutosha kufanya kile walichodhamiria baada kukaa kimya kwa miaka yote 7 bila kufanya chochote kupitia team yao.

morning glory3

“kwa sasa tupo tayari kuachia alibamu yetu ya kwanza ambayo itatoka katika tenzi za injili albamu hiyo itakuwa na nyimbo 12 ambazo zitakuwa na vionjo vya kusifu na kuabudu, nyimbo zetu zitakuwa na ladha tofauti sana ambayo haijawahi kusikika popote, kwa sasa tupo kwenye hatua za awali za kuadaa albamu hiyo. Mambo yatakapokuwa tayari tutawafikishia taarifa kadiri siku zinavyozidi kwenda” alisema Osward.

(Habari na Picha - Jane Mhina)