MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 19 MACHI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA NI 'TUTUNZE MAZINGIRA'

  1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
  1. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti.
  2. Leo kutakuwa na ibada ya maombi hapa Usharikani kuanzia saa 9.00 alasiri. Aidha siku ya alhamisi  tarehe 23.03.2017 saa 11.30 jioni kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi hapa usharikani ambacho kitaongozwa na mtumishi Baraka Mbise toka KKKT Ubungo. Wote mnakaribishwa.
  1. Jumatano ijayo tarehe 22/03/2017 saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada kama kawaida ya Kwaresma.  Zamu za wazee itakuwa ni kundi la pili. Aidha  Ratiba nzima ya ibada siku za jumatano imebandikwa kwenye ubao wa matangazo mlango mkuu kwenye bahasha za Ahadi na nje Karibu na duka letu la vitabu.
  1. Kwaya ya Umoja itaendelea na mazoezi kama kawaida kwa ajili ya maandalizi ya Kantate siku ya Jumanne ijayo tarehe 21/03/2017 saa 11.00 jioni.  Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria na kufika kwa wakati.
  1. Familia ya Bwana na Bibi Michael T. Moshi wamepata zawadi ya mtoto wa kiume tarehe 06/03/2017 katika hospitali ya Seliani Arusha. Baba, mama na mtoto wanaendelea vizuri.
  1. Jumapili ijayo tarehe 26/03/2017 katika ibada ya pili familia ya Mama Cristina Nzali watamshukuru Mungu kwa mambo mengi ambayo Mungu amewatendea.

Neno: Zab. 138:1-3, Wimbo: Kutoka Kwaya Kuu

  1. Jumamosi ijayo tarehe 25/03/2017 saa 3.00 asubuhi kutakuwa na mkutano wa VICOBA ya Wajane na Wagane. Wahusika wote wanakaribishwa na kuzingatia muda.
  1. Jumapili ijayo tarehe 26/03/2017 tutashiriki chakula cha Bwana. Hivyo ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi.  Washarika tujiandae
  1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
  • Upanga: Watangaziana
  • Kinondoni:  Kwa Mama Hilda Rwezaula
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: watashiriki ibada hapa usharikani
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Theophilus Mlaki
  • Oysterbay/Masaki: watashiriki ibada hapa usharikani
  • Tabata: Watangaziana
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
  • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi G. Mnyitafu
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Prof na Bibi Adolph Lawson