MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 26 JUNI, 2022

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

WITO WA KUINGIA UFALME WA MUNGU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti. 

3. Matoleo ya Tarehe 19/06/2022

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

6. Jumapili ijayo tarehe 03/07/2022 ni siku ya Sadaka ya Harambee ya kituo chetu cha Kiroho Kiharaka. Hivyo ibada itakuwa ni moja, itakayoanza saa 2.00 asubuhi. Washarika wote tujiandae na kuiombea siku hiyo.

7. Jumanne ijayo tarehe 28/06/2022 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya Baraza la Wazee na Ijumaa tarehe 01/07/2022 Kikao cha Baraza Wazee. Wajumbe mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kwa wakati.

8. Leo tarehe 26/06/2022 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.

9. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

Kwa mara ya kwanza tunatangaza Ndoa zitakazofungwa tarehe 16/07/2026 

SAA 10:00 JIONI

Bw. Victor Remmy Machange na Bi. Jesca Edward Mollel

Matangazo mengine ya Ndoa yapo kwenye ubao wa Matangazo.

10. NYUMBA KWA NYUMBA

* Masaki na Oyserbay: Kwa Bwana na Bibi Mchangila

* Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe

* Mjini kati: watafanya njia ya Mtandao.

* Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo

* Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaura

* Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi George Msuya

* Upanga: Kwa Mama Nsiah Kimaro

11. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki