Date: 
17-03-2023
Reading: 
Mwanzo 2:15

Hii ni Kwaresma 

Ijumaa asubuhi tarehe 17.03.2023

Mwanzo 2:15

Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.

Tutunze mazingira;

Mungu alifanya kazi ya kuiumba dunia, na baada ya kumaliza uumbaji huo siku ya saba (Mwz 2:2) akamuumba mwanadamu kama tunavyosoma;

Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Ndipo sasa kwenye somo letu tunaona Mungu akimtwaa huyo mtu na kumweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.

Ujumbe huu unakuja kwetu asubuhi ya leo, kwamba Mungu alituumba akatuweka duniani, tuilime na kuitunza dunia. Kutunza dunia ni wajibu wetu. Tunaitunza dunia kwa kulinda na kutunza mazingira tuliyomo. Tusipotunza mazingira hatuutunzi uumbaji, tunatenda dhambi. 

Ijumaa njema.

Heri Buberwa