Date: 
03-01-2023
Reading: 
Nahumu 1:2-8

Jumanne asubuhi tarehe 03.01.2022

Nahumu 1:2-8

[2]BWANA ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; BWANA hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; BWANA hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira.

[3]BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.

[4]Yeye huikemea bahari na kuikausha, pia huikausha mito yote; Bashani hulegea, na Karmeli; hulegea nalo ua la Lebanoni.

[5]Milima hutetema mbele zake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele za uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake.

[6]Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.

[7]BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.

[8]Lakini kwa gharika ifurikayo atapakomesha kabisa mahali pake, na kuwafuatia adui zake hata gizani.

Anza yote katika jina la Yesu Kristo;

Nabii Nahumu anaandika juu ya ghadhabu ya Mungu kwa watu wasiomtii. Bwana ni mwingi wa hasira kwa watu wasiolitii neno lake. Nabii Nahumu anaonesha ghadhabu ya Mungu kwa kuandika kuwa hakuna awezaye kusimama mbele ya ghadhabu ya Mungu. Nabii Nahumu anaonesha wema wa Bwana, maana yeye hutaka watu wamfuate, na wasipomfuata ndipo huwa na ghadhabu.

Tunakumbushwa kuwa ghadhabu ya Bwana ipo kwa watenda dhambi, ili tutubu na kubadilika. Kwa tafsiri pana, q inatukumbusha kuwa hukumu ya Mungu ipo kwa watenda dhambi. Tutaiepuka ghadhabu ya Mungu kwa kuishi katika neno la Mungu na kufanya yote aliyoagiza katika jina la Yesu Kristo.

Siku njema.