Date: 
27-07-2023
Reading: 
Zaburi 86:11-17

Alhamisi asubuhi tarehe 27.07.2023

Zaburi 86:11-17

11 Ee Bwana, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako;

12 Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele.

13 Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.

14 Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia; Mkutano wa wakatili wamenitafuta roho. Wala hawakukuweka Wewe Mbele ya macho yao.

15 Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.

16 Unielekee na kunifadhili mimi; Mpe mtumishi wako nguvu zako, Umwokoe mwana wa mjakazi wako.

17 Unifanyie ishara ya wema, Wanichukiao waione na kuaibishwa. Kwa kuwa Wewe, Bwana, Umenisaidia na kunifariji.

Uchaguzi wa busara;

Zaburi ya 86 ni Sala ya Daudi akiomba Bwana aisikie sala yake. Sehemu tuliyosoma ni ombi la Daudi kwa Bwana kuwa amfundishe njia yake, naye anaahidi kuishika. Daudi anakiri fadhili za Bwana, ambazo ameziona maishani mwake. Daudi anaomba ulinzi wa Mungu, kuwakabili wote wasiomtakia mema. Anaomba fadhili za Bwana zisiondoke kwake milele. 

  • Daudi anafanya sala yake kwa Bwana. Anachagua kwa busara.
  • Daudi anaomba ulinzi wa Mungu, anachagua kwa busara 
  • Daudi anakiri fadhili fadhili za Bwana, na anaomba zisiondoke kwake. Anachagua kwa busara.
  • Anaomba Bwana amsaidie kuwaepuka watu wabaya, anachagua kwa busara.

Tunaweza kusema Daudi anaomba kuongozwa na Bwana maisha yote, popote. 

Daudi anakuwa mfano bora kwetu, kwamba tuombe na kutamani kuongozwa na Bwana maishani mwetu. Huu ndiyo uchaguzi wa busara katika maisha ya Imani. Amina.

Alhamisi njema 

Heri Buberwa