Date: 
13-09-2023
Reading: 
Marko 14:3-9

3 Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake.
4 Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwani kupoteza marhamu namna hii?
5 Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung'unikia sana yule mwanamke.
6 Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamtaabisha? Amenitendea kazi njema;
7 maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.
8 Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko.
9 Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.

Uwakili wetu kwa Bwana;

Yesu akiwa Bethania, mwanamke anampaka (Yesu) mafuta ya marhamu kichwani. Wapo waliochukizwa na jambo hilo, wakisema marhamu hayo yangeuzwa ili hela wapewe maskini! Katika mstari wa saba Yesu anawaambia hao watu waliochukizwa na jambo hilo kuwa wanao maskini siku zote, na wangeweza kuwahudumia wakati wote.

Yesu anasema kuwa yule mwanamke alitenda jambo muhimu sana kwa kumpaka Yesu mafuta, jambo ambalo ni la kukumbukwa daima. Tutakumbukwa hata uzima wa milele tukidumu katika imani kwa kutenda mema. Amina.


Siku njema!

----------------------------------------

Heri Buberwa 
Mlutheri