Date: 
14-11-2023
Reading: 
Isaya 50:4-9

Jumanne asubuhi tarehe 14.11.2023

Isaya 50:4-9

4 Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.

5 Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma.

6 Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.

7 Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya.

8 Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni nani atakayeshindana nami? Na tusimame pamoja; ni nani aliye hasimu yangu? Na anikaribie basi.

9 Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia; ni nani atakayenihukumu kuwa mkosa? Tazama hao wote watachakaa kama vazi; nondo atawala.

Mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka;

Sura ya 50 inaanza kwa Bwana kutoa onyo kwa Taifa lake, kwa kutofuata maagizo yake. Sasa katika somo hili Nabii Isaya anasema alivyotumwa na Bwana kuleta ujumbe wa neema kwa wote. Ukisoma mbele anawambia watu walivyomkosea Mungu;

Isaya 50:10-11

10 Ni nani miongoni mwenu amchaye Bwana, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la Bwana, na kumtegemea Mungu wake.
11 Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.

Isaya anahoji nafasi ya watu wa Mungu katika kumfuata Bwana. Ni watu waliomkosea Bwana. Isaya anawapa ujumbe wa kumtumainia Bwana na kulitegemea jina lake. Ujumbe wangu kwako leo ni kumtumainia Yesu Kristo na kulitegemea jina lake, ili uwe na mwisho mwema. Amina.

Siku njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri