Date: 
17-11-2023
Reading: 
Ayubu 21:1-5

Ijumaa asubuhi tarehe 17.11.2023

Ayubu 21:1-5

1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

2 Yasikizeni sana maneno yangu; Jambo hili na liwe faraja yenu.

3 Niacheni, nami pia nitanena; Tena nikiisha nena, zidini kudhihaki.

4 Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu? Nami kwa nini nisikose kusubiri?

5 Niangalieni, mkastaajabu, Mkaweke mkono kinywani.

Mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka;

Ayubu alipitia mateso makali sana alipojaribiwa na shetani. Alipoteza mali na familia. Lakini katika yote hayo Ayubu hakutenda dhambi;

Ayubu 1:21-22

21 akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.
22 Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.
Ayubu alipitia ushawishi uliomtaka kumuacha Bwana aliyemuabudu. Yeye hakuona sawa. 

Somo la leo asubuhi hii linamuonesha Ayubu akisema kumngoja Bwana. Hakujali anapitia nini, bali Bwana ndiye aliyemwamini na kumtumaini. Wito kwetu leo ni kuvumilia katika Bwana kwa njia ya Yesu Kristo, ndipo tutaurithi uzima wa milele. Amina.

Ijumaa njema.

Heri Buberwa