MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 26 NOVEMBA, 2023

SIKU YA BWANA YA MWISHO KABLA YA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

MAANDALIZI KWA UZIMA WA MILELE

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 19/11/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Jumamosi ijayo tarehe 02/12/2023 kutakuwa na ibada ya ubarikio kwa watoto wa Kipaimara kwa Kingereza. Ibada itaanza saa 3.00 asubuhi Washarika tuiombee siku hiyo.

6. Leo tarehe 26/11/2023 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.

7. Jumapili ijayo tarehe 03/12/2023 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

SHUKRANI: JUMAPILI IJAYO TAREHE 03/12/2023

IBADA YA PILI SAA 3.00 ASUBUHI

 • Familia ya Marehemu Josephat Ndaksoi Makundi watamshukuru Mungu kwa kwa mambo mengi aliyotutendea

Neno: Isaya 41:10, , Wimbo: Mission Praise no. 200

8. NDOA ZA WASHARIKA

MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 16/12/2023 

SAA 08:00 MCHANA

 • Bw. Wilbert Exaud Kwayu na Bi. Simona Mrinji Gadi 

SAA 9.00 ALASIRI

 • Bw. Modest Mero na Bi. Vicky Kawedi Shayo

MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 09/12/2023 

SAA 07:00 MCHANA

 • Bw. Nguzo Heriel Kida na Bi. Catherine Ngarami Mushi 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

8. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

 • Oysterbay na Masaki: Kwa Bw & Bi Kimweri
 •  
 • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bw & Bi Charles Lyimo
 •  
 • Mjini kati: Watatangaziana
 • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bw & Bi Rweikiza
 • Kinondoni: Watatangaziana
 •  
 • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bw & Bi George Msuya
 •  Upanga: Kwa Mr & Mrs Happiness Nkya
 • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bw & Bi Victor Kida

11. Zamu: Zamu za wazeeni ni Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.