Date: 
05-12-2023
Reading: 
Mathayo 22:41-46

Jumanne asubuhi tarehe 05.12.2023

Mathayo 22:41-46

41 Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo?

42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.

43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,

44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?

45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?

46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.

Bwana analijia Kanisa lake;

Yesu anawauliza Mafarisayo kuhusu Kristo, kuwa ni nani? Mafarisayo wanasema ni mwana wa Daudi. Yesu anaendelea zaidi kuwauliza kuhusu uhusiano wa Kristo (yeye Yesu) na Daudi, kwamba inakuwaje Daudi anamuita Bwana, halafu Kristo ni mwana wa Daudi! Hakuna aliyeweza kujibu neno.

Ilikuwa vigumu kwa Mafarisayo kumjibu Yesu kwamba alikuwa mwana wa Mungu na mwokozi wa ulimwengu maana hawakumwamini. Pamoja na mafundisho na ishara zote, bado hawakuamini. Ndiyo maana walikuwa na kigugumizi. Kutokuamini kwao hakuzuia chochote, maana aliendelea na kazi yake hadi mwisho. Huyu Kristo ndiye atarudi tena kulichukua Kanisa. Jiandae kumpokea. Amina.

Jumanne njema

Heri Buberwa