Date: 
08-12-2023
Reading: 
Yohana 10:7-10

Ijumaa asubuhi tarehe 08.12.2023

Yohana 10:7-10

7 Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.

8 Wote walionitangulia ni wevi na wanyang'anyi; lakini kondoo hawakuwasikia.

9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.

10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Bwana analijia Kanisa lake;

Yesu anawaambia Wayahudi kuwa yeye ni mlango wa zizi la kondoo, asiyeingia kupitia mlango huo ni mwizi! (10:1-6) Hawakuelewa maana ya maneno haya, ndipo Yesu akaendelea na mstari wa saba kwamba yeye ni mlango wa kondoo. Yesu anajitambulisha kama mlango wa kondoo ambaye mtu akipita kwake ataokoka. Akitoka kwa mlango wake atapata malisho. Ukiendelea kusoma kuanzia mstari wa 11 unaona Yesu akijitambulisha kama Mchungaji mwema autoaye uhai wake kwa ajili ya kondoo.

Yesu alitumia mfano wa Mchungaji wa kondoo kujitambulisha kama Mwokozi wa ulimwengu. Wachungaji wa kondoo walikaa machungani wakiongoza kondoo siku zote. Hivyo alitumia mfano huo kuwaambia kuwa yeye ndiye Mchungaji na kiongozi wao, zaidi ya yote yeye ndiye Mwokozi wao. 

Yesu ndiye Mwokozi wetu.

Tujiandae kumpokea. Amina.

 

Heri Buberwa