Date: 
14-12-2023
Reading: 
Isaya 59:16-21

Alhamisi asubuhi tarehe 14.12.2023

Isaya 59:16-21

16 Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia.

17 Akajivika haki kama deraya kifuani, na chapeo cha wokovu kichwani pake, akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi yake, naye alivikwa wivu kama joho.

18 Kadiri ya matendo yao, kwa kadiri iyo hiyo atawalipa, ukali kwao wampingao, malipo kwa adui zake; naye atavirudishia visiwa malipo.

19 Basi, wataliogopa jina la Bwana toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya Bwana.

20 Na Mkombozi atakuja Sayuni, kwao waachao maasi yao katika Yakobo, asema Bwana.

21 Tena katika habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema Bwana; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema Bwana, tangu leo na hata milele.

Yesu anakuja katika Utukufu wake;

Somo la asubuhi hii linapatikana katika sehemu ya tatu ya kitabu cha Isaya, ambapo kuna ujumbe wa Taifa la Mungu baada ya kutoka uhamishoni. Somo linaonesha ukuu wa Bwana na nguvu yake kwa watu wake. Mstari wa 21 unaonesha ahadi ya Bwana, kwamba ataendelea kuwapa watu wake neno lake na kuwalinda hata milele. Yaani hata baada ya kutoka Babeli uhamishoni na kurudi katika nchi yao, Bwana aliahidi kuwa nao daima.

Ahadi ya Mungu tangu kale hata sasa ni kuwalinda na kuwatunza watu wake. Katika kuwalinda na kuwatunza watu wake, neno lake ni muhimu sana. Yaani sisi tulio Kanisa la Mungu tunakumbushwa kudumu katika neno lake, ili tuwe na mwisho mwema katika yeye. Amina.

Alhamisi njema 

Heri Buberwa