Date: 
19-12-2023
Reading: 
Luka 3:1-3

Hii ni Advent 

Jumanne asubuhi tarehe 19.12.2023

Luka 3:1-3

1 Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Uyahudi, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene,

2 wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani.

3 Akafika nchi yote iliyo karibu na Yordani, akihubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi,

Itengenezeni njia ya Bwana;

Luka anaelezea Yohana Mbatizaji alivyoikaribia nchi yote karibu na Yordani akihubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Ukiendelea kusoma unaona Yohana akitangaza habari za kuja kwa Kristo;

Luka 3:4-6

4 kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
5 Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patalainishwa;
6 Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu.

Yohana anaposema itengenezeni njia ya Bwana anawaalika waamini kuiandaa mioyo yao kumpokea Kristo ajaye kuwakomboa. Ni mwaliko kwetu kuishi maisha ya toba ili Bwana akae kwetu siku zote. Kama Yohana anavyosema, tuandae mioyo yetu kumpokea Kristo, ndipo tutauona wokovu wa Mungu. Amina.

Jumanne njema.

 

Heri Buberwa