Date:
21-10-2024
Reading:
Waebrania 10:37-39
Jumatatu asubuhi tarehe 21.10.2024
Waebrania 10:37-39
37 Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.
38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
39 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.
Tuishindanie Imani katika Kristo Yesu;
Mwandishi wa waraka kwa Waebrania anaandika kwamba bado kitambo kidogo, yeye ajaye atakuja hatakawia. Anatoa ujumbe wa kurudi kwa Yesu kulichukua Kanisa, akisisitiza kuishi kwa Imani katika Kristo Yesu. Anawatoa wasomaji wake wasiwasi akiwaambia wasisite katika njia ya ufuasi, bali wamuishie Kristo aliye Mwokozi wa ulimwengu.
Msingi wa somo ni kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili, pale mwandishi anaposema "yeye ajaye atakuja, hatakawia". Ni ujumbe kuwa hatma yetu iko kwa Yesu ambaye atarudi kuhukumu ulimwengu na kulichukua Kanisa. Ni kwa msingi huo mwandishi anatusisitizia kuishindania imani katika Kristo Yesu ili tuwe na mwisho mwema. Amina.
Uwe na wiki njema
Heri Buberwa