Jumamosi asubuhi tarehe 09.08.2025
Isaya 62:1-5
1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.
2 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.
3 Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.
4 Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula;kwa kuwa Bwana anakufurahia ,na nchi yako itaolewa.
5 Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.
Tunaitwa kuzaa matunda mema;
Somo la asubuhi ya leo ni uthibitisho wa wokovu kwa Taifa la Mungu. Ni ujumbe wa Mungu kwa watu wake baada ya kuwa wamekombolewa kutoka uhamishoni, Bwana akiitangaza neema na haki yake kwa kuwaokoa watu wake kama alivyokuwa amewaahidi. Bwana anendelea kuwaahidi watu wake kuuona Utukufu wa Bwana, na nchi yao kuendelea kutajwa kwa mema.
Kwa hiyo leo asubuhi tunasoma juu ya ahadi ya Mungu juu ya Israeli, kwamba pamoja na kuwaokoa toka uhamishoni bado asingewaacha. Mstari wa nne unatoa ahadi kabisa ya kutoachwa, kutokuwa wakiwa. Kumbe pamoja na kutuokoa dhambini, Kristo anatufurahia daima akitutuma kuitenda kazi yake kwa uaminifu kwa kumzalia matunda. Amina
Jumamosi njema
Heri Buberwa