Date: 
14-08-2025
Reading: 
Luka 6:12-16

Alhamisi asubuhi tarehe 14.08.2025

Luka 6:12-16

12 Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.

13 Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume;

14 Simoni, aliyemwita jina la pili Petro, na Andrea nduguye, na Yakobo na Yohana, na Filipo na Bartolomayo,

15 na Mathayo na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Simoni aitwaye Zelote,

16 na Yuda wa Yakobo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyekuwa msaliti.

Uchaguzi wa busara;

Asubuhi hii tunasoma Yesu akiwaita wanafunzi wake na kuchagua kumi na wawili miongoni mwao ambao aliwaita Mitume. Kabla ya kuwachagua, tunaona Yesu akienda mlimani kuomba, anakesha usiku kucha akimwomba Mungu. Bila shaka ni baada ya maombi Yesu alipata kuwachagua wale Mitume kumi na wawili. 

Uchaguzi alioufanya Yesu ulikuwa baada ya maombi ya usiku kucha. Kumbe Yesu anatukumbusha kuomba katika yote tufanyayo. Tukiomba kwa jina lake anafanya, kama yeye alivyoomba akawachagua wanafunzi. Kwa Yesu kuomba kabla ya uchaguzi wa Mitume, ni kutukumbusha kuwa makini katika kufanya maamuzi yanayohusu maisha yetu. Maamuzi ya muhimu kabisa kuliko yote ni kumwamini Yesu. Amina

Alhamisi njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com