Date:
03-09-2025
Reading:
Isaya 2:11-12
Jumatano asubuhi tarehe 03.09.2025
Isaya 2:11-12
11 Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
12 Kwa maana kutakuwa siku ya Bwana wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.
Mungu huwapinga wenye kiburi;
Isaya anatoa ujumbe kwa Taifa la Mungu juu ya adhabu ya kuburi. Ukisoma kuanzia mstari wa 8 unaona wakionywa kuhusu uovu katika kutukuza kazi bunafsi, ibada ya sanamu na mengine kama hayo, ambayo Isaya anasema pasipo toba hakuna msamaha. Katika somo la asubuhi hii Isaya anasema kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, ni Bwana pekee atatukuzwa. Isaya anakazia kwamba kiburi na majivuno vitashushwa chini.
Israeli walikuwa wanapewa ujumbe wa kuzingatia ili wasipelekwe uhamishoni. Sehemu tuliyosoma asubuhi ya leo inawaambia kuwa wanyenyekevu, waache kiburi maana kiburi na majivuno vitashushwa chini. Ujumbe huu unatujia asubuhi ya leo, kwamba tuache kiburi, maana Mungu huwapinga wenye kiburi na kuwapa wanyenyekevu neema. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650