Date: 
10-10-2025
Reading: 
Yohana 11:38-41

Ijumaa asubuhi tarehe 10.10.2025

Yohana 11:38-44

38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.

39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.

40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?

41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.

42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.

43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.

44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.

Mungu hututunza kwa uwezo wake mkuu;

Sura ya 11 ya Injili ya Yohana husimulia kufa na kufufuliwa kwa Lazaro. Yesu alikuwa amefuatwa na ndugu zake Lazaro akamponye wakati akiwa hawezi. Yesu hakuwahi kuelekea Lazaro alipo, akisema ni kwa ajili ya Utukufu wa Mungu kudhihirika. Tunaona Yesu akifika kwenye kaburi la Lazaro na kuamuru jiwe liondolewe. Jiwe liliondolewa, Yesu akafanya sala na kumuita Lazaro atoke nje. Lazaro akatoka kaburini.

Ikumbukwe kwamba Lazaro alikuwa amelala kaburini kwa siku nne hadi anafufuliwa na Yesu. Yesu alidhihirisha kwamba yeye ni Bwana, na siyo mtu wa kawaida kama ambavyo wengi walidhani. Itukumbushe ukuu wa Mungu, kwamba yeye anaweza kutuongoza katika maisha yetu katika hali zote. Tumtegemee daima, maana yeye hututunza kwa uwezo wake mkuu. Amina

Ijumaa njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com