Umoja wa wanawake Azania Front wakiongozwa na Mwenyekiti wa umoja huo Apaisaria Kilewo uliofuatana na Mama Askofu Erica Malasusa, walitembelea kituo cha kulelea watoto yatima na watoto wenye mazingira hatarishi cha DonBosco kilichopo Kimara Suka Dar es salaam.

Mama Erika Malasusa alitoa neno la ufunguzi wa maongezi mafupi kati ya umoja wa wanawake na watoto wa kituo hicho pamoja na uongozi wa kituo hicho, Neno lilitoka katika kitabu cha Yohana 13: 34-35

Kituo cha Don Bosco kilianzishwa mwaka 1998, na Evans Tegete, ambaye ndio mkurengenzi wa kituo hicho, mpaka sasa kituo kina watoto wasiopungua 88 wa rika mbalimbali.

Kituo hiki ni kutuo pekee ambacho kimekuwa kikisimamia maadili kwa watoto ambao wanaishi katika kituo hicho, mpaka sasa kituo kimesomesha wanafunzi 26 ambao wamemaliza ngazi ya chuo kikuu, mbali na hao kuna wanafunzi 21 ambao bado wanaendea na chuo pia kuna wanafunzi 9 ambao wako kidato cha nne na cha tano.

Mbali na umoja wa wanawake kupeleka zawadi za sikukuu kama mchele, sukari, mafuta, mikate,sabuni, majani ya chai chumvi n.k . pia umoja huo unasomesha wanafunzi saba wa ngazi ya Sekondari na chuo.

Mkurugenzi wa kituo hicho aliushukuru umoja huo kwa kusema kwamba bila wakina mama hawa asingeweza kufika hapo alipofiki kwasababu wamekuwa wakimtia sana moyo na kumuombea ili aendelehe kuwatunza watoto wenye uhitaji.

”Bila kinamama wa Azania Front naisi hiki kituo kisinge wepo tena maana wakinamama hawa wamekuwa wakinapa sapoti kubwa sana ambayo sikutegemea kabisa lakini kwa uwezo wa Mungu wakinamama wameweweza kunitia moyo na kunisaidia kwa namna mbalimbali kama kuniletea misaada kuwasomesha baadhi ya watoto katika ngazi tofautitofauti nawashukuru sana ninawaombea kwa Mungu muendelee kushikamana na umoja wa kina mama huo wa Azaniafront udumu milele”

don bosco 2015 dec 01

Baadhi ya Vijana ambao wanaosomeshwa na kituo hicho

don bosco 2015 dec 02

Baadhi ya watoto ambao wako kidato chja tano wakinyoosha mikono juu

don bosco 2015 dec 03

Baadhi ya watoto na wakinamama wa azania front wakiwa wanasikiliza jambo kwa makini

don bosco 2015 dec 04

Hili ni jengo la kituo cha Don Bosco

don bosco 2015 dec 05

Katibu, mama msangi akifurahia jambo na mtoto

don bosco 2015 dec 06

Kijana wa kituo cha Don Bosco akisukuru kwa niaba ya wanzake ujio wa umoja wa

wanawake kwa zawadi za christmas na kuwatembelea

don bosco 2015 dec 07

Mama Apaisalia kilewo akifurahia jambo

don bosco 2015 dec 08

Mama Apaisalia KIlewo akisema jambo kwa watoto wa kituo cha Don Bosco

don bosco 2015 dec 09

Mama askofu Erica Malasusa akiandaa somo, kushoto ni Elly Swai na kulia ni Hilda

Rwanshane 

don bosco 2015 dec 10

Mama askofu Erica Malasusa akifunga kwa sala

don bosco 2015 dec 11

Mama Askofu Erica Malasusa akifungua kwa sala 

don bosco 2015 dec 12

Mama Askofu Erica Malasusa akitoa neno kwa watoto wa kituo cha Don Bosco na umoja

wa wanawake Aania Front

don bosco 2015 dec 13

Mkurugenzi wa kituo cha Don Bosco Evance Tegete akiwakaribisha wakinamama wa

Azania Front

don bosco 2015 dec 14

Mkurugenzi wa kituo cha Don Bosco MR Evance Tegete akibadilisha jambo na katibu

Theuda msangi na mjumbe wa umoja wa wanawake Azania Front

don bosco 2015 dec 15

Nsarry hoza msimamizi wa watoto wanafunzi akito shukrani kwa niaba ya uongozi wa

kituo

don bosco 2015 dec 16

Umoja wa kinamama wakiwasili katika kituo cha Don Bosco

don bosco 2015 dec 17

Vijana ambao wanaingia kidato cha kwanza mwakani

don bosco 2015 dec 19

Zawadi za christmas ambazo watoto wameletewa na umoja wa kinamama Azania Front