Event Date: 
21-10-2022

Siku ya Ijumaa, tarehe 14 Octoba 2022 ilifanyika semina ya siku moja kwa Baraza Jipya la Wazee wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral. Semina hiyo iliyolenga kuweka mipango na mikakati itakayoongoza baraza hilo katika utendaji wake wa kazi za kila siku iliongozwa na Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dk Alex Malasusa.

Miongoni mwa waliohudhuria semina hiyo ni Dean Chediel Lwiza, Chaplain Charles Mzinga, Mchungaji Joseph Mlaki pamoja na Wazee wote wa Kanisa waliochaguliwa hivi karibuni kwa ajili ya kuhudumu katika usharika wa Kanisa Kuu Azania Front kwa kipindi cha miaka minne (2022-2026).

Baadhi ya Picha kutoka kwenye Semina hiyo.

Baba Askofu Dk Alex Malasusa akizungumza wakati wa Semina hiyo 

Wazee wa Kanisa na Viongozi wengine wakifuatilia semina hiyo 

Wazee wa Kanisa na Viongozi wengine wakifuatilia semina hiyo 

Picha ya pamoja ya Wazee wa Kanisa na Viongozi wengine wakiwa na Baba Askofu Dk Alex Malasusa 

Baba Askofu Dk Alex Malasusa akisalimiana na baadhi ya Wazee wa Kanisa waliohudhuria semina hiyo